Siku ya Quds: Wapalestina waendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Israel

Kiswahili Radio 37 views
Huku dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds, Wapalestina wanaendeleza mapambano na muqawama dhidi ya dhulma na uonevu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kalenda ya matukio ya dunia, imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem). Mwaka huu siku hii inasadifiana na Mei 22.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.

Utawala ghasibu wa Israel unawakandamiza Wapalestina na kukalia ardhi zao kwa mabavu, ukiwemo mji wa Quds, kwa himaya ya madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu.

Taifa la Palestina linasisitiza kuwa, maadamu kuna dhulma na uonevu basi amani katu haiwezi kupatikana katika eneo.

 

Add Comments