Mufti wa Tanzania Samahat Sheikh Abubakar Zubeir atoa mwongozo kuhusu Corona

Kiswahili Radio 6 views
Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir atoa mwongozo kuhusu Corona, Waislamu Kenya walaani mauaji ya polisi wa nchi hiyo dhidi ya baba na watoto wake wawili

Ripoti ya matukio ya Kiislamu inahusu mwongozo uliotolewa na Mufti wa Tanzanua Sheikh Abubakar Zubeir Ali leo Ijumaa kuhusiana na ugonjwa wa Corona ambapo amemshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuitikia Dua za watanzania. Taarifa iliyosomwa na msemaji wa mufti Sheikh Hassan Chizenga, mufti ametoa muongozo huo kufuatia habari ya kupungua maambukizi ya Corona nchini Tanzania. Amesema kuwa, kutokana na maendeleo hayo, vyuo vya dini ya Kiislamu ambavyo vina watu wazima,  wanafunzi warejee kama ilivyotangazwa na serikali. Ama watoto wadogo waendelee kusubiri mpaka serikali itakapotoa maelekezo mengine. Ama nukta nyingine ni kwamba, mikusanyiko ya kidini na kiibada nje ya nyumba za ibada kama vile kumbi na mfano wake zitakazowahusu watu wazima zitaendelea kwa kuzingatia taratibu za Afya zilizowekwa.

Add Comments