Maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamekubaliana kwamba, kuanzia tarehe Mosi Julai watayaunganisha maeneo ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi na ardhi zainazokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Suala hilo limepingwa vikali na jamii ya kimataifa.
Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetangaza kuwa, mpango wa utawala haramu wa Israel wa kuyatwaa maeneo zaidi ya Ukingo wa Magharbi wa Mto Jordan utazusha machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati.