Uvunaji wa maua ya tiba ya echium nchini Iran

Kiswahili Radio 32 views
Maua ya echium yana faida za kipekee za kitiba katika kukabiliana na magonjwa mengi mbalimbali.

Maua hayo yanatumika kutengeneza dawa za kutibu magonjwa mengi kama mafua. Maua hayo yanapokaushwa hutumika kutengenezea chai. Maua ya echium yanastawi zaidi katika maeneo ya milimani ingawa yanapandwa pia katika maeneo ya makazi ya watu kwa viwango vidogo. 

Maua hayo huvunwa mwishoni mwa mwezi Mei katika maeneo ya milimani ya mkoa wa Golestan nchni Iran kwa muda wa siku 20.

Add Comments